WASAIDIZI WA KISHERIA KWA AJILI YA HAKI ZA MAZINGIRA

Kituo cha Sera na Utafiti- Mpango wa Haki za Mazingira wa Namati Utangulizi na Maelezo ya Jumla ya Mwongozo wa Utendaji Maeneo mengi ya dunia, bila kujali viwango vyao vya maendeleo ya kiuchumi, yapo katika ukingo wa mgogoro mkali wa kimazingira. Katika maeneo haya, shughuli za miradi ya uzalishaji kama vile mashamba makubwa, uchimbaji madini na maendeleo ya viwanda zimezorotesha hali za kiuchumi, kijamii na afya za jamii jirani na zile za mbali pia. Sheria na tasisi zao imara za kitaifa na kimajimbo zilizopo kwa ajili ya ulinzi na usimamizi wa malighafi zimebakia kwenye karatasi na ukiukwaji wa sheria umekuwa na athari kubwa kwenye maisha ya ya jamii, afya, upatikanaji wa ardhi na maisha bora. Mwongozo wa utendaji wa Namati na CPRS wa wasaidizi wa kisheria wa Haki za Mazingira ni hatua moja iliyolenga kuziba mwanya huu wa utekelezaji wa kimazingira. Mwongozo huu unatoa mbinu kwa wahamasishaji wa jamii, wanaharakati na makundi ya wananchi waache kutaja tu matatizo na waanze kuchukua malalamishi yanayoshughulikiwa na taasisi za kimazingira. Mwongozo huu ni matokeo ya miaka minne ya kazi iliyofanywa na wasaidizi wa kisheria wa Mpango wa Haki za Mazingira wa CPRS- Namati ili kusaidia jamii athirika kuandikisha malalamishi na kutafuta suluhu katika kesi zaidi ya 150 za ukiukwaji huko India. Tunatarajia kwamba mwongozo huu utayasaidia mashirika ya mitaa na makundi ya kijamii kuishughulikia migogoro ya kimazingira na kuwatafutia utatuzi wale walioathirika. This resource is also available in FrenchOriyaHindiGujaratiKannada, and Bahasa Indonesian.